Na Ben Barka
Mjini Baghdad kuna kaburi la
jemadari wa majeshi ya Kiingereza yaliyovamia
Jenerali Sir Stanley Maude
aliyeuawa wakati wa mashambulizi hayo. Maandishi juu ya kaburi hilo yanamnukuu akisema
“tulikuja hapa siyo kama wavamizi bali kama wakombozi.” Hii si hadithi ya
mwaka
2003 bali ni 1917. Wakati huo “wakombozi” hao walioongozwa na Maude waliwaua
raia
10,000
wa Iraq kwa kutumia silaha za kemikali. Huo ndio “ukombozi” wa Iraq wa mwaka
1917
Iraq
kwa hiyo ina historia ndefu ya kuvamiwa na majeshi ya kigeni. Bush (mkubwa na
mdogo) hawakuwa wa kwanza
kuvamia
nchi hiyo.
Mwaka
huu majeshi ya Marekani na Uingereza yalipoivamia Iraq (kinyume cha sheria za
kimataifa) waliwaua zaidi ya raia
10,000
na askari 20,000. Hii ndiyo gharama waliyolipa Wairaq ili “wakombolewe” na
majeshi ya uvamizi.
Vyombo
vya habari vimekaa kimya kuhusu gharama hii.
Ni tofauti na
watu 3000 waliouawa katika ushambulizi wa
zao
zilikuwa zikirudia habari hizo usiku na mchana. Lakini hatuambiwi chochote
kuhusu halaiki ya Wairaq waliouawa
kutokana
na silaha za maangamizi za Marekani.
Yale
mabomu ya kutawanya (cluster bombs) utayaitaje kama si ya mangamizi. Ndizo
zilizowauwa maelfu ya watoto,
wazee na wanawake nchini
ya
raia waliokuwa wakishangilia kuangushwa kwa sanamu ya Saddam.
Kuna
habari nyingine ambazo zinafichwa. Hatuambiwi kwa nini baada ya “ukombozi”
ulioshangiliwa na wananchi wa Iraq
majeshi
ya uvamizi yanaendelea kuuawa. Wangapi tunajua kuwa tangu Iraq “ikombolewe” na
tangu Bush atangaze ushindi
mnamo
Mei majeshi yake yamekuwa yakifa zaidi kuliko wakati wa ushambulizi wenyewe.
Badala
yake tunaambiwa kuwa bado kuna wafuasi wachache wa chama cha Baath ambao
wanaleta ukorofi. Kama ni
hivyo
basi wale Washia wa kusini nao pia sasa wamejiunga na chama cha Baath?
Hawatuambii
ukweli kuwa Wairaq wa sehemu zote, Shia na Sunni, sasa wanapinga kwa nguvu
uvamiaji na utawala wa
Marekani
uliopewa jina bandia la utawala wa muungano. Hata hiyo serikali iliyoteuliwa na
Marekani inakataliwa na wananchi
kwa
sababu ni serikali bandia ya vikaragosi. Ndiyo maana baadhi yao wamelazimika
kujiuzulu na wengine wameuawa.
Ndiyo
maana haipiti hata siku moja bila ya majeshi ya uvamizi kushambuliwa nchini
Iraq. Habari hizi hupewa umuhimu
mdogo
na badala yake magazeti na TV zimekuwa zikirudia propaganda za Bush
Naye
Bush anaendelea kutuambia kuwa kuna wakorofi wachache tu ambao wanapinga
demokrasia na mageuzi. Ukweli
ni
kuwa “wakorofi” hawa ndiyo wanaomtia kiwewe na kumfanya akimbilie Umoja wa
Mataifa na kuomba msaada wa
majeshi
ya kimataifa.
Na
vyombo vya habari vinaendelea kumkariri Bush bila ya maswali. Vinatumika kama
vyombo vya kuwapumbaza raia wa
Marekani.
Matokeo yake ni kuwa raia wa kawaida wa Marekani anaamini kuwa Saddam ndiye
aliyepanga uvamizi wa New
York
mnamo 2001, kuwa yeye amekuwa akishirikiana
na Osama bin Laden na Al Qaida.
Raia
huyu wa kawaida anaamini kuwa Saddam alikuwa tishio kubwa kwa usalama wa
Marekani. Hizi ni nguvu za vyombo
vya
habari katika kuwapumbaza raia. Wanaokataa kupumbazwa huitwa wahaini na maadui
wa taifa. Wengi wao wamefungwa
bila
ya kuhukumiwa au kufunguliwa mashtaka. Huo ndio uwezo uliopewa serikali ya Bush
katika nchi hii inayojiita ya
demokrasia
na utawala wa sheria.
Ni
watu wachache tu kama akina Profesa Chomsky, John Pilger na Edward Said
(marehemu) ambao wamekuwa msitari wa
mbele
katika kuandika waziwazi wakifichua ukweli.
Wamekuwa
wakionyesha kuwa Marekani ni nchi ya kibeberu ambayo ina historia ndefu ya
kuzivamia nchi za ulimwengu wa
tatu
na kupora utajiri wake. Uvamizi huu wa Iraq ni wa 73. Historia hii ya uvamizi
inaanzia pale wazawa wa Marekani
walipouawa na
kuporwa nchi
Na
kila uvamizi unapofanyika basi kazi ya serikali huwa ni kuwapumbaza wananchi
kwa kuficha ukweli. Marekani ilipotaka
kushambulia
utawala wa Spain huko Amerika ya kusini walianza kwa kusingizia kuwa Spain
ilikuwa imezamisha meli ya
Marekani
iitwayo Maine. Baada ya hapo magazeti yakarudia uwongo huu na wananchi
wakatayarishwa kwa mashambulizi.
Halafu
mnamo miaka ya 1960 Marekani ilieneza uwongo mwengine kuwa Umoja wa Kisovieti
(USSR) ulikuwa ukiunda
makombora
makubwa yaliyokuwa yameelekezwa Marekani. Waandishi wakapewa nyaraka bandia nao
wakaeneza uwongo
mkubwa
ili kuwatayarisha wananchi kwa matumizi ya mabilioni kwa kuunda silaha za
kisasa ili kukabiliana na “tishio la
kikomunisti.”
Marekani
walipotaka kuivamia Jamhuri ya Kisosashilisti ya Vietnam walianza kwa kueneza
uwongo kuwa nchi hiyo ilikuwa
imeshambulia
manowari mbili za Marekani katika Ghuba ya Tonkin. Magazeti yakarudia mara kwa
mara uwongo huu na
wananchi
wakapandisha mori wakimtaka Rais Johnson aishambulie
Mnamo
miaka ya 1980 Rais Reagan alibuni visingizio vya kuwashambulia wananchi wa
Amerika ya Kusini waliokuwa
wakipigana
dhidi ya madikteta vibaraka wa Marekani. Mfano mmoja ni nchi ndogo ya Nicaragua
ambako wanaukombozi
wa
Sandinista wakiongozwa na Daniel Ortega waliiangusha serikali dhalimu ya Somoza
iliyokuwa ikiungwa mkono na
Marekani.
Marekani
ikabuni uwongo kuwa Sandinista walikuwa ni tishio kwa Marekani. Ndipo Reagan
alipowakusanya vibaraka
magaidi
waitwao Contra na kuwapa silaha na fedha ili kupindua utawala wa Sandinista. Matokeo
ya ugaidi huu wa Reagan
ni
wananchi 70,000 kupoteza maisha
Na
hayo si ya Reagan tu. Leo hii utawala wa Geroge W Bush unaendelea kutoa hifadhi
kwa wauaji, watesaji, wateka nyara
ndege na
magaidi kutoka
maalum iliyopo Fort Benning (Georgia).
Halafu
Bush anadai kuwa anapigana na ugaidi duniani. Naye anaungwa mkono na propaganda
zinazoendeshwa na tajiri
mkubwa
Rupert Murdoch anayemiliki mtandao wa magazeti na TV kama Fox. Idhaa hii kazi
yake kubwa imekuwa ni
kumpigia
vigelegele Bush na kuwapumbaza wananchi.
Hali
hii ya upigaji debe itaenelea kuwa mbaya. Kwani hivi sasa tume ya utangazaji
huko Marekani inaongozwa na Michael
ambaye ni
mtoto wa waziri wa mambo ya nje Colin Powel. Tume hii inakusudia kubadili sheria ili kuruhusu makampuni
machache
yaweze kuhodhi vyombo vya habari.
Matokeo
yake ni kuwa Fox pamoja na makampuni mengine manne yatakuwa yanadhibiti
asilimia 90 ya TV za kitaifa nchini
Marekani.
Huo eti ndio uhuru wa habari.
Licha
ya TV njia nyingine kubwa ya kueneza propaganda ni Internet. Hivi sasa asilima
60 ya mitandao hii inatawaliwa na
makapuni 14
Hao
ndio watakaoamua aina ya habari zitakazoenezwa. Huo uhuru wa habari tunaoupigia
kelele haupo chini ya utandawazi
na
ubeberu. Ni ndoto ya mchana. Ndiyo maana ukweli huwa unafichwa na uwongo
huenezwa.
Kwa
mfano ni wangapi kati yetu tunaelewa kuwa uvamizi na uporaji huu wa Iraq ni
uvamizi wa 73 katika historia ya ubeberu
wa
Marekani. Ukiachia haya mashambulizi ya waziwazi kuna oparesheni za siri zaidi
ya 100 dhidi ya mataifa ya kigeni.
Kuanzia
mbinu za kuwaangusha akina Mohammed Mosadeq wa Iran na Salvador Alliende wa
Chile hadi majaribio ya
kumuua
Rais Fidel Castro, ubeberu wa Kimarekani umekuwa daima ukitumia silaha
kuzikandamiza nchi za dunia ya tatu.
Hiyo
ni khulka ya ubeberu iliyokuwepo tangu karne na karne.
Vyombo
vya habari vya magharibi vimekuwa vikificha ukweli huu. Kama vile Iraq
iliposingiziwa kuwa inahatarisha usalama
wa
dunia. Mfano mwengine ni pale Marekani ilipodanganya ulimwengu kuwa Spain
ilikuwa imeshambulia manowari ya
Kimarekani
iitwayo Maine. Ndipo Marekani ilipotumia kisingizio cha kuishambulia
Spain.
Pia
mnamo 1960 waandishi walipewa nyaraka za uwongo zikionyesha kuwa eti Umoja wa
Sovieti (USSR) ulikuwa unaunda
makombora
yenye uwezo mkubwa kushinda Marekani. Ndipo Marekani ilipopata kisingizio cha
kuunda silaha kubwa ili
kukabiliana
na hilo “tishio” la Kisovieti. Uwongo
huu ulienezwa na waandishi bila ya kudadisi.
Ni
kama vile walivyoeneza uwongo kuwa wanaharakati wa Vietnam walikuwa wamezamisha
manowari mbili za Marekani
katika
ghuba ya Tonkin. Hawakudai kuonyeshwa ushahidi wala hawakudadisi. Badala yake
tahariri zilicharuka kutaka
Vietnam
nayo ishambuliwe.
Wimbo
huo ndio aliokuwa akiutaka Rais Johnson ambaye aliutumia kama kisingizio cha
kuishambulia Vietnam kwa mabomu
ya
sumu na silaha nyingine za maangamizi. Kwani Marekani ni wamiliki na watumaiaji
wakubwa wa silaha za maangamizi.
Haya
hayasemwi na vyombo vya propaganda.
Na
hivi karibuni tumeona jinsi Rais Bush na Waziri Mkuu Tony Blair walivyobuni
uwongo na jinsi walivyowadanganya raia
wao
kabla ya kuishambulia Iraq. Uchunguzi wa
Jaji Hutton huko London hivi sasa unaonyesha kiasi gani unafiki na uzandiki
ulivyokuwa
ukitawala propaganda za kivita.
Mengi
zaidi yatafichuka wakati wananchi wa Marekani nao watakapofanikiwa kuwa na
uchunguzi wao. Hizi zitakuwa ni
skandali
kubwa kushinda zile za Watergate.
Colin
Powell alidiriki kusimama mbele ya Baraza la Usalama (UN) na kutoa vielelezo
vya uhange na picha za kubuni akidai
eti
alikuwa na uhakika Saddam alimiliki silaha za maangamizi. Alipoambiwa tumuachie
basi Bw Blitz na wataalamu wenzake
waendelee
na uchunguzi wao huko Iraq akasema Blitz anaregarega mno.
Leo
hii Marekani baada ya kuivamia Iraq imeshindwa kufichua hizo silaha za
maangamizi kwa kisingizio eti Saddam alikuwa
mjanja
na huenda amezificha mahali pasipojulikana. Kama ni hivyo basi mbona wakati ule
Marekani ilijifanya ilikuwa na
uhakika
kuwa inajua zilipo silaha hizo? Kama Saddam alikuwa na hizo silaha iweje
akubali kupinduliwa bila ya kuzitumia?
Aliziunda
kama pambo tu?
Ukweli
ni kuwa walitudanganya. Tarehe 9 July Donald Rumsfeld alipoulizwa alitabasamu
na kusema kuwa Marekani kamwe
haikuwa
na ushahidi wa kutosha. Aliungwa mkono na naibu wake Paul Wolfowitz ambaye alisema kuwa silaha za
maangamizi
ni sababu pekee ya kuwafanya watu waunge mkono uvamizi wa Iraq.
Sasa
hata Bush anaungama kuwa hakukuwa na ushahidi wowote kuwa Saddam alihusika kwa
njia yeyote na mashambulizi
ya
New York ya 2001. Hata hivyo gazeti moja linaripoti kuwa asilimia 69 ya
Wamarekani wanagali wanaendelea kuamini
kuwa
Saddam alihusika. Inaonyesha jinsi kasumba inavyofanya kazi huko Marekani.
Tarehe
11 Septemba kila mwaka serikali ya Marekani huwakumbuka watu 3000 waliokufa
kule New York. Wakati huohuo
zaidi
ya raia 10,000 wamekufa nchini Iraq kutoka na uvamizi wa Marekani. Hawa
hawakumbukwi. Malaki ya wananchi
wa
Iraq pia wamekufa katika muda wa miaka
12 kutokana na vikwazo vya uchumi. Hawa hawakumbukwi.
Wakati
huohuo hali inazidi kuwa mbaya kwa majeshi ya Marekani huko Iraq. Kwa mujibu wa
gazeti la New York Times
la
tarehe 22 Septemba jumla ya askari wa Marekani 304 wamekufa tangu kuanza kwa
uvamizi. Likinukuu ripoti ya Pentagon
gazeti
hilo linasema tangu Bush kutangaza ushindi tarehe 1 Mei zaidi wa askari 165
wamekufa. Zaidi ya 1100 wamejeruhiwa
vibaya.
Katuni
iliyochorwa katika gazeti moja huko Marekani inaonyesha makaburi maalum ya wale
askari waliokufa wakati wa
kuivamia
Iraq. Lakini ubavuni kuna makaburi ya wale askari wanaoendelea kufa baada ya
kumalizika kwa vita vya uvamizi.
Haya
makaburi ya pili yamefurika na nafasi sasa haitoshi. Kwani kila siku idadi ya
askari wa Marekani wanaendelea
kushambuliwa
na kufa huko Iraq. Mimi sijaona TV za magharibi zikionyesha maiti hizi zikirudishwa
nyumbani na kuzikwa.
Msemaji
wa majeshi ya Marekani, Luteni Kanali George Krivo, alisema kuwa kila siku
majeshi yake huko Iraq
yanashambuliwa
mara kumi hadi ishirini. Alisema, “tutaendelea kushambuliwa, mashabulizi haya
yanazidi kuwa ya hali ya juu.”
Bush
na Blair walipokuwa wakijiandaa kuivamia Iraq wapelezezi na majasusi
waliwatahadharisha kuwa kwa kufanya
hivyo
tishio la ugaidi dunianai lingeongezeka. Huko Uingereza kuna kamati ya
usalama iitwayo Intelligence and Security
Committee (ISC) inayoongozwa
na mbunge wa chama cha Labour aitwaye Ann Taylor.
Kamati hii ilitoa onyo hili na kusema kuwa serikali ilikuwa inawadanganya wananchi.
Kamati ilimwambia Blair kuwa
hakukuwa na
ushahidi wowote kuwa Sadam na Osama walikuwa wakishirikiana. Pia ISC ilisema
kuwa si kweli
alivyosema
Blair kuwa Saddam alikuwa na silaha za maangamizi ambazo zinegeweza kushambulia
nchi za magharibi katika
muda wa
dakika 45 tu.
Pia
huko Uingereza kuna kamati ya ya pamoja ya mashirika ya ujasusi iitwayo Joint
Intelligence Committee (JIC). Hii
inaunganisha
majasusi kutoka MI6, MI5, GCHQ, Defence Intelligence na kadhalika. Tarehe 10
February mwaka huu JIC
ilimuonya
Blair kuwa kuishambulia Iraq kutaongeza ugaidi na wakasema kuwa Saddam hakuwa
tishio kwa usalama.
Blair
badala ya kusikiliza ushauri huu wa wapelelezi aliendelea kuwahadaa umma. Licha
ya habari hizi za JIC na ISC Tony
Blair
aliliambia bunge tarehe 18 Machi kuwa Saddam alikuwa anahatarisha usalama wa
ulimwengu kutokana na silaha zake
za
maangamizi.
Ingawa
kulikuwa na upinzani mkubwa, wengi wa wabunge walidanganyika na kumuunga mkono
Blair. Sasa baada ya siri
hizi
ya ISC na JIC kuwekwa wazi Bw Blair ameachwa kwenye mataa. Tayari uchaguzi
mdogo wa Brent East hivi majuzi
umeonyesha
kuwa chama cha Labour kimeanza kuporomoka, kwani kimepoteza kiti kilichokuwa
kinashikilia kwa muda mrefu.
Tarehe
1 Mei Rais Bush alitangaza kuwa vita vya kumg’oa Saddam vilimalizika. Ilikuwa
ni sherehe kubwa. Lakini kama
ilivyotabiriwa
na wapepelezi, huo haukuwa mwisho wa mapigano. Kwa kweli tunaweza kusema vita
ndio kwanza vimepamba
moto.
Kama
tulivyona, majeshi ya Marekani yanashambuliwa karibu mara ishirini kila siku. Na
haipiti siku bila ya askari wa
Marekani
kuawa. Siku hizi TV zao hata hazionyeshi habari hizi. Kwa mfano BBC inatanguliza
habari za mkutano wa IMF
huko
Dubai. Habari inayofuata ni ile ya kuuawa kwa askari wawili wa Marekani na
kujeruhiwa 13 nchini Iraq.
Marekani
ina askari 140,000 huko nao wanajiuliza lini watarudi nyumbani. Rumsfeld
alipowatembelea aliulizwa suala hilo
naye
akajibu kuwa itabidi waendelee kukaa huko na kuhimili mashambulizi ya Wairaq.
Inasemekana
ili kudhibiti mashambulizi haya ni lazima kuwa na angalao majeshi 500,000. Ndivyo
walivyofanya huko
Vietnam
na mwishowe wakalazimika kufyata mkia na kukimbia.
Lakini
suala ni kuwa watapata wapi askari laki tano. Siyo tu askari hao hawatakubali
kwenda huko bali gharama itakuwa
ni
kubwa mno. Bush anajaribu kuzishawishi nchi zingine zipeleke majeshi yao. Labda
akina Museveni wanaweza kuwapeleka
askari
wao. Mtumikie kafiri upate mradi wako ndiyo sera ya Museveni na wenzake.
Lakini
Bush anachotaka ni kuungwa mkono na mataifa makubwa kama Ufaransa au Ujerumani. Nao wamesema kuwa
hawataunga
mkono mpaka Iraq ikabidhiwe kwa Umoja wa Mataifa. Bush naye hakubali kuachia
ngawira ya Iraq. Labda
atakachofanya
Bush ni kuunda jeshi la Wairaq wenyewe. Lakini majeshi haya ya vibaraka
hayatakuwa na usalama.
Wananchi
wanataka Wamarekani waachie madaraka na waondoke.
Huenda
ikawa kama ilivyokuwa Vietnam. Huko Vietnam waliunda majeshi ya vibaraka ambao
walishambuliwa vibaya na
majeshi
ya kizalendo. Na ndipo ikabidi kutuma majeshi ya Marekani “kuwasaidia.” Nao pia
walishindwa kukabiliana na
majeshi
ya ukombozi.
Halafu
kuna gharama kubwa ya vita inayoelemea wananchi wa Marekani. Hivi sasa Marekani
inatumia $ 2 bilioni kila mwezi
huko
Iraq. Tangu kuanza mashambulizi
zimekwishatumika $ 70 bilioni. Bado Bush anahitaji fedha nyingine $ 87 bilioni.
Uvamizi
wa Iraq utakuwa umewagharimu wananchi wa Marekani karibu $ 160 bilioni. Huo ni
mzigo mkubwa. Katika historia
ya
Marekani haijawahi kutumia kiasi kama hiki cha fedha katika nchi yeyote ya
kigeni. Mara ya mwisho baba yake Bush
aliposhambulia
Sasa kwa
kumwaga fedha zote hizo katika uvamizi wa
aidi ya
dola nusu trilioni. Yaani bajeti ya Bush itakuwa na
upungufu wa $ 500,000,000,000.
Si ajabu chama cha Democrat
kimeanza kumshambulia Bush kuwa anatumia fedha nyingi zaidi huko
ya
elimu na matibabu nchini Marekani. Ni hao hao Democrats
waliokuwa wakipeperusha bendera ya Marekani na
kumuunga
mkono Bush sasa wanampinga.
Ndiyo
kampeni ya urais hiyo. Mwakani Bush itabidi agombee tena na tayari kura za
maoni zinaonyesha kuwa watu walio
wengi
wamemchoka. Hata Blair naye aliyeungwa mkono na wabunge wengi sasa anaonekana
ni mzigo kwa chama cha
Labour.
Katika mkutano mkuu wa chama hicho wajumbe walikatazwa kuzungumzia suala la
Iraq.
Wengi
wanatabiri kuwa ushambulizi wa Iraq matokeo yake ni kuanguka kwa Bush na Blair.
Uvamizi
wa Iraq umewatumbukia nyongo Bush na Blair. Kwa ripoti nyingine iliyotolewa
hivi karibuni inasema kuwa hakuna
ushahidi
kuwa Iraq ilikuwa na silaha za maangamizi.
Kikundi
cha watu 1400 kikiongozwa na CIA kitwacho Iraq Survey Group (ISG) kimekuwa
kifanya utafiti huko kwa muda
wa
miezi sita. Ripoti yake imewasilishwa kwa Bush na Blair. ISG inakanusha ripoti
ya National Intelligence Estimate (NIE)
ya
Oktoba 2002 iliyodai kuwa Saddam alikuwa akimiliki mamia ya tani ya silaha za
sumu.
Profesa Richard Stoll wa Chuo Kikuu cha Rice huko Marekani alisema:
“Ukiwakamata au kuwaua
wapiganaji 1000 wa Al Qaeda haimaanishi kuwa kikundi hicho kimedhoofika kwa
kupungua
idadi
wanaotaka
kujiunga nacho.”
Hivyo
ndiyo historia itakavomkumbuka Bush. Johnson aliangushwa na
Published by
email: harakatips@hotmail.com